Ee Bwana Wangu

Ee Bwana Wangu
ChoirMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerMarcus Mtinga
Musical Notes
Time Signature4
4
Music KeyG Major
NotesOpen PDF

Ee Bwana Wangu Lyrics

Ee Bwana wangu na muumba wangu,
Wema wako wanitia nguvu kuongea nawe
Ee Mungu wangu u tumaini langu,
Wewe ni mlinzi mwaminifu wa maisha yangu
Ninajua wazi ya kwamba, unanipenda upeo Bwana
Wewe ni mwali mwangavu wa roho yangu
Ndiwe tegemeo pekee, ni kimbilio langu, Bwana,
Chanzo cha uzima wangu, na ngome yangu

 1. Kama sio wewe Bwana kukaa pamoja nami,
  Wanadamu waliponishambulia wangenimaliza
  Ulikuwa ngao yangu, Mwokozi wa roho yangu
  Sina budi kusema asante naomba usiniache
 2. Nilipokuita Bwana uliitika mapema
  Katika taabu zangu zote ulituma jeshi lako
  Umenifanya imara imani sikuitupa
  Na leo tazama niko hapa kutaja uwezo wako
 3. Ni kweli naona wazi huruma uliyo nayo
  Umenisamehe dhambi zangu ingawa ni chafu sana
  Umenitoa shimoni umenifuta machozi
  Naomba unipake mafuta nieneze sifa zako
 4. Nitakupa nini Bwana kama shukrani zako,
  Kwa ukarimu uliotenda, katika maisha yangu
  Umeniokoa Bwana, minyororo imekatwa
  Naomba usinitupe Bwana, shetani ananiwinda

Also recorded by St. Paul's Students Choir, University of Nairobi