Login | Register

Sauti za Kuimba

Ee Maria Lyrics

EE MARIA

Ee Maria, Mama wa Mungu,
utuombee sisi Wanao

 1. Mwenye heri, wewe Bikira Maria,
  tunakusalimu, Maria.
 2. Uliyemchukua aliyekuumba,
  tunakusalimu, Maria.
 3. Umetuzalia Mkombozi wetu,
  tunakusalimu, Maria.
 4. Uliyekingiwa dhambi ya asili,
  tunakusalimu, Maria.
 5. Uliyepalizwa mbinguni kwa Mungu,
  tunakusalimu, Maria.
 6. Mama wa Kanisa Mama yetu mwema,
  tunakusalimu, Maria.
 7. Wastahili sifa za vizazi vyote,
  tunakusalimu, Maria.
Ee Maria
CATEGORYBikira Maria
 • Comments