Ee Mungu Wangu Umenichunguza

Ee Mungu Wangu Umenichunguza
Performed bySt. Peter Oysterbay
CategoryZaburi
Views9,342

Ee Mungu Wangu Umenichunguza Lyrics

  1. { Ee Mungu wangu umenichunguza,
    Ukanifahamu nilivyo mimi } *2
    { Wayafahamu matendo yangu
    Nikiketi au kusimama, wewe unanijua mimi } *2

  2. Nikiwa kazini waniona - wewe unanijua mimi
    Wewe wajua mawazo yangu -
    Ningali bado nafikiria -
    Nikifanya mabaya gizani -
  3. Wanizunguka kila upande -
    Waniwekea mkono wako -
    Maarifa hayo ni ya ajabu -
    Siwezi kuyaelewa mimi -
  4. Nikimbie wapi mbali na wewe -
    Niende wapi nikajifiche -
    Nikipanda juu wewe uko -
    Nikiwa safarini waniona -
  5. Umeniumba mwili na roho -
    Ulinitengeneza tumboni -
    ` Hata kabla sijazaliwa -
    Uwezo wako ni wa ajabu -