Ee Mungu Wangu Nifundishe

Ee Mungu Wangu Nifundishe
Performed by-
CategoryTafakari
Views7,629

Ee Mungu Wangu Nifundishe Lyrics

  1. Ee Mungu wangu unifundishe
    Unifundishe kuwa mkarimu
    Unifundishe kukutumikia kama unavyostahili
    Kama unavyostahili,
    Kutoa wala nisihesabu gharama
    Kukubali mateso bila kunung'unika
    Nitumike pasipo kutafuta pumziko

  2. Nifanye kazi kwa moyo bila kutafuta ujira
    Ee Mungu nisaidie nijitoe kwa kazi yako
  3. Nisaidie kujua nafanya mapenzi yako
    Nisije nikajikwa kwa kukosa uaminifu
  4. Mimi askari wa Yesu ee Bwana uniimarishe
    Nipigane hata kufa nikitetea jina lako