Ee Mungu Wangu Nifundishe Lyrics

EE MUNGU WANGU NIFUNDISHE

Ee Mungu wangu unifundishe
Unifundishe kuwa mkarimu
Unifundishe kukutumikia kama unavyostahili
Kama unavyostahili,
Kutoa wala nisihesabu gharama
Kukubali mateso bila kunung'unika
Nitumike pasipo kutafuta pumziko

  1. Nifanye kazi kwa moyo bila kutafuta ujira
    Ee Mungu nisaidie nijitoe kwa kazi yako
  2. Nisaidie kujua nafanya mapenzi yako
    Nisije nikajikwa kwa kukosa uaminifu
  3. Mimi askari wa Yesu ee Bwana uniimarishe
    Nipigane hata kufa nikitetea jina lako
Ee Mungu Wangu Nifundishe
CATEGORYTafakari
  • Comments