Ekaristia Takatifu

Ekaristia Takatifu
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)

Ekaristia Takatifu Lyrics

 1. Ekaristia takatifu ni mwili na damu yake Yesu
  Aliyesulubiwa msalabani ili kutukomboa
  Jioni Alhamisi katwaa mkate,
  (Pia) Divai kawapa wanafunzi
  (Ili) wanywe kwa ukumbusho wake


  Njooni njooni wateule (wote)
  Njooni tumwabudu Kristu katika sakramenti
  (Ndugu) njooni njooni tumwabudu Yesu
  Njooni njooni tumwabudu Kristu katika sakramenti

 2. Tujongee taratibu tukale karamu takatifu
  Aliyotuachia Yesu Kristu kwa ukarimu wake
  Chakula cha uzima [Na] kinywaji cha roho
  (Hili) ni fumbo alilotuachia
  Tuadhimishe kwa ukumbusho wake
 3. Ekaristi takatifu huleta neema ya Mbinguni,
  Huleta mapatano kati yetu naye muumba wetu
  Walio na imani wanayo baraka
  (Hadi) milele wanalo hakikisho
  (Lile) la kushiriki kwa utukufu wake