Enendeni Msiogope
| Enendeni Msiogope | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
| Album | Nakaza Mwendo (Vol 19-20) |
| Category | Injili na Miito (Gospel) |
| Composer | Fr. Mutajwaha |
| Views | 5,737 |
Enendeni Msiogope Lyrics
{ Enendeni, nendeni msiogope
Lihubiri neno duniani pote, nendeni }*2- Enyi wanafunzi wangu mimi nawatuma
Mataifa yote nendeni mkahubiri
Nendeni kwa moyo wote wala msiogope
Shikeni vyema shauri ninalowapa ee! - Enjili hii viumbe vyote visikie
Ili mapenzi ya Baba yatimilike
Nyumba, anasa na mali havina nafasi
Ondokaneni na hivyo nimewatuma ee! - Dhiki hatari na shida havitawaweza
Giza na hila za mwovu vitayeyuka
Elewa kwamba mimi nipo nanyi daima
Ondoeni shaka kwani sitawaacha ee! - Nanyi mkishatimiza niliyowamuru
Posho kupata na taji mtavalishwa
Itakuwa heri gani Mbinguni kufika
Enzi nitakayopewa kuwarithisha ee!