Enyi Mataifa
| Enyi Mataifa | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Mbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4) |
| Category | Zaburi |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 4,400 |
Enyi Mataifa Lyrics
Enyi mataifa, Mshukuruni Mungu wa Miungu (Mungu),
Mshukuruni Mungu kwa kuwa yeye ni mwema kwetu
Kwa furaha kuu -
Pigeni ngoma kinanda na kinubi nalo zeze
Ni shangwe leo -
Watu wote waimbe kwa furaha na kucheza -
Mmh mmh mshukuruni Mungu wa miungu mshukuruni
Kaweza Bwana -
Sisi nasi twaimba aleluya aleluya- Fadhili za Bwana zinadumu kwao wamchao,
Fadhili za Bwana zinadumu kwao wamchao - Na rehema zake kwetu sisi kweli za milele,
Na uaminifu wake wadumu milele yote - Mwimbieni Bwana Mungu yeye astahili sifa,
Na fadhili zake Bwana Mungu yeye za milele.