Enyi Watu Wote Pigeni Makofi
Enyi Watu Wote Pigeni Makofi | |
---|---|
Performed by | Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha |
Album | Nikupe Nini Mungu Wangu |
Category | Entrance / Mwanzo |
Composer | S. B. Mutta |
Views | 17,499 |
Enyi Watu Wote Pigeni Makofi Lyrics
{ Enyi watu wote pigeni makofi,
Enyi watu wote pigeni makofi,
Pigieni Bwana Mungu wetu,
Shangilieni kwa vigelegele } *2- [ s ] Enyi watu pigeni makofi, mpigieni Mungu,
Pigeni kelele kwa sauti ya shangwe - Kwa kuwa Bwana aliye juu, ni mwenye kuogofya,
Ndiye mfalme mkuu wa dunia yote - Bwana atawatiisha watu, wote wa nchi yake
Na mataifa chini ya miguu yake - Bwana Mungu wetu amepaa, kwa sauti ya shangwe
Amepaa kwa sauti ya baragumu - Enyi watu wote mwimbieni, Bwana naam imbeni
Mwimbieni mfalme na mshangilieni
Unaweza imbwa kama wimbo wa kuingia (mwanzo), zaburi na pia Siku kuu ya kupaa kwa Bwana.