Habari Tuliyoleta

Habari Tuliyoleta
Alt TitleNi Nani Aliyesadiki
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CategoryZaburi
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,961

Habari Tuliyoleta Lyrics

  1. Je! Je! Ni nani aliyesadiki habari hii tuliyoleta
    Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani
    Maana alikua mbele zake kama mche kama mche mwororo
    (Na kama) kama mzizi katika nchi kavu
    { Alidharauliwa na kukataliwa na watu
    Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko } *2

  2. Ni kama mtu ambaye watu humficha uso
    Aliyedharauliwa, hakuhesabiwa kitu
    Hakika kayachukua, na masikitiko yetu,
    Amejitwika huzuni, huzuni, huzuni yetu
  3. Lakini tulidhania, yeye kuwa amepigwa
    Ya kuwa yeye kapigwa kapigwa yeye na Mungu
    Bali alijeruhiwa, yeye kwa makosa yetu
    Alichubuliwa yeye, pia kwa maovu yetu
  4. Adhabu amani yetu, ilikuwa juu yake,
    Kwa kupigwa kwa sisi, sisi sote tumepona
    Sisi ni kama kondoo, kondoo tumepotea
    Tumegeukia njia, kila mtu njia yake