Login | Register

Sauti za Kuimba

Habari Tuliyoleta Lyrics

HABARI TULIYOLETA

@ J. C. Shomaly

Je! Je! Ni nani aliyesadiki habari hii tuliyoleta
Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani
Maana alikua mbele zake kama mche kama mche mwororo
(Na kama) kama mzizi katika nchi kavu
{ Alidharauliwa na kukataliwa na watu
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko } *2

 1. Ni kama mtu ambaye watu humficha uso
  Aliyedharauliwa, hakuhesabiwa kitu
  Hakika kayachukua, na masikitiko yetu,
  Amejitwika huzuni, huzuni, huzuni yetu
 2. Lakini tulidhania, yeye kuwa amepigwa
  Ya kuwa yeye kapigwa kapigwa yeye na Mungu
  Bali alijeruhiwa, yeye kwa makosa yetu
  Alichubuliwa yeye, pia kwa maovu yetu
 3. Adhabu amani yetu, ilikuwa juu yake,
  Kwa kupigwa kwa sisi, sisi sote tumepona
  Sisi ni kama kondoo, kondoo tumepotea
  Tumegeukia njia, kila mtu njia yake
Habari Tuliyoleta
ALT TITLENi Nani Aliyesadiki
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYZaburi
REFIs. 53
MUSIC KEYD Major
SOURCEUniversity of Nairobi
 • Comments