Hakuna Aliye Sawa
| Hakuna Aliye Sawa | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
| Album | Nikiziangalia Mbingu (vol 18) |
| Category | Zaburi |
| Composer | Basil Lukando |
| Views | 6,539 |
Hakuna Aliye Sawa Lyrics
Hakuna aliye sawa naye Mungu
Aketiye mahali patakatifu pake
Anayetutendea mengi makuu ya ajabu
Basi yatupasa sote tumshukuru *2- Ardhi yarutubishwa na mvua zinyeshazo-
Kazi hiyo ni ya nani?
Angalieni mazao yastawi mashambani-
Kazi hiyo ni ya nani? - Watoto wanazaliwa na kukua nazo afya-
Kazi hiyo ni ya nani
Wazazi wapata riziki kuwahudumia-
Kazi hiyo ni ya nani - Safari zawa salama bila misukasuko-
Kazi hiyo ni ya nani
Tumshukuru kwa kuwa yeye ndiye mwenye haki-
Mapenzi yake yatimizwe