Harusi Kidededede
Harusi Kidededede Lyrics
- { Bwana harusi na bibi harusi, leo mmefunga ndoa ya maisha,
Kaeni kwa amani kidededede } * 2
Upendo wenu umedhihirika
Uyani kwenu bamba ishini tototo
Uzuri wenu hauna kifani
Uyani kwenu bamba ishini tototo
Na nyumba yenu imebarikiwa
Uyani kwenu bamba ishini tototo ooo
- Jitulize mjisikie sukari, siku ya leo ni yenu,
Furahini, mmepambwa maua mnapendeza
- Bwana arusi kwanza wachangamka, bibi arusi chachawa,
Chezacheza, penzi lenu leo limekamilika
- Mapenzi yenu yote yatasitawi, hakika yatasitawi,
Yatamea, kama ule mwerezi wa Lebanoni
- Baraka zake Mungu ziwashukie, kaeni pasipo shida,
Siku zote nyumba yenu iwe hekalu la Mungu.