Harusi ya Kwanza
Harusi ya Kwanza |
---|
Performed by | - |
Category | Harusi |
Views | 4,286 |
Harusi ya Kwanza Lyrics
- Arusi ya kwanza ilifanywa shambani
Mungu aliumba Adam na Hawa
Na aliwaambia wakae wawili
Mzae watoto mjaze dunia
[Kuna shida kweli]
Mtu akioa miaka mitatu tano
matusi dharau zikaja nyumbani
[Msipovumilia] mtaangamia
Bwana anasema mjaze dunia
- Ewe bibi harusi na Bwana harusi
Sasa mmefunga pingu za maisha
Lakini mjue Shetani yu karibu
Anabisha hodi kuja awatenganishe
- Vikwacha nyumbani nazo mtazipata
Taabu magonjwa nyumbani mtapata
Lakini mjue hayo ni maisha
Yote yatokeapo mshukuruni Mungu