Haya Karibuni
Haya Karibuni Lyrics
Haya wapendwa wote mwaalika kwa karamu
Kushiriki utamu, utamu wa karamu
karamu ya Bwana *2
Amka ndugu yangu Bwana Yesu ametuita
Tukale mwili wake pia tukanywe damu yake
(twende) simama simama simama
Simama umpokee ee changamka changamka
Changamka changamka akujaze neema zake
- Karamu ya mapendo karamu safi na takatifu,
Mwaalikwa wapendwa ili mpokee
- Wenye mioyo safi Mwokozi sasa ametuita,
Kwa moyo safi twende wote tupokee
- Tutubu dhambi zetu tushiriki karamu ya Bwana
Kwa moyo safi twende wote tupokee
- Ni mapendo makubwa Mwokozi yeye katulinda
Tuleni siku zote tufike kwake