Haya Tazameni

Haya Tazameni
Alt TitleAmeweza
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumHaya Tazameni (Vol 21)
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerBernard Mukasa
Views27,668

Haya Tazameni Lyrics

  1. Haya tazameni nyinyi wenyewe
    Mungu wangu mwenye nguvu ametenda yote
    Hata magumu yasiyofanyika
    Mungu wangu mwenye nguvu ametenda yote

    Ameweza - huyo ameweza yametimia
    Ameweza - huyo ameweza yametimia
    Oh Bwana Mungu kaweza - huyo ameweza yametimia
    Yasiyowezekana - huyo ameweza yametimia
    Yote ameyatenda - huyo ameweza yametimia
    Ameweza - huyo ameweza yametimia

  2. Maji yaliyomwagika kabisa -
    Ameyazoa yakajaa upya -
  3. Katikati ya bahari ya Shamu -
    Israeli kapita kwa miguu -
  4. Nipofukiwa shimo la zege -
    Kulipokucha kaniweka huru -
  5. Vilema vyangu nilipomwonyesha -
    Amevigusa vikapona mara -
  6. Nitapaza sauti kilimani -
    Dunia yote isikie haya -