Hebu Jiulize
Hebu Jiulize Lyrics
{Hebu jiulize lingetolewa tangazo leo
Ya kwamba kila apumuaye
na ailipie pumzi avutayo } *2
Ni nani angejificha asilipe kodi,
Ni nani angesema yeye ni masikini,
Ni nani angekwepa kwani yeye ni tajiri
Ni nani angekuwa kweli mtu wa kiburi
Ni nani angekwepa kweli kulipia kodi (nasema)
Ni nani angependa kunyang'anywa uhai wake * 2
- Tazama sasa majirani zako wote,
Hakuna unayeongea naye
Kwani unawadharau
kwa kuwa wao hawana fedha kama zako
Hebu tazama baadhi ya ndugu zako,
Hupendi hata kuwaona kwako
Unawakana kwa kuwa, wao ni maskini,
tena unawaona ni wachafu.
- Kwa nini hivyo, biashara zako,
wewe unawaajiri wafanya kazi
Tena ni wachapa kazi na mwisho wa mwezi,
huwafichia eti wameiba
Hebu tazama wapoteza fedha nyingi,
unapokuwa baa na marafiki
Kwa ajili tu ya anasa, na kuwasaidia,
maskini kwako ni hasara
- Jitafakari, fungua na legeza moyo wako
kwa kuwajali wasiojiweza
Na wenye shida mbalimbali, na sio kuegeza
Hazina ya moyowe kwa shetani.