Heri Ninyi Lyrics

HERI NINYI

@ A. O. Dimoso

{ Heri ninyi watakapo washtumu
Na kuwanenea kila neno baya } *2
{ Lakini furahini sana (sana) na kushangilia
Kwa kuwa dhawabu yenu kubwa Mbinguni } *2

 1. Watawasaliti ninyi ili mpate dhiki
  Watawakamata ninyi na kuwapiga sana
  Kwa ajili ya jina langu
 2. Watawazushia ninyi maneno ya uwongo
  Watawahukumu ninyi jinsi watavyotaka
  Kwa ajili ya jina langu
 3. Watawafuata ninyi ili wawasakame
  Kwa maana mtasifiwa kwa kila mfanyacho
  Kwa ajili ya jina langu
Heri Ninyi
COMPOSERA. O. Dimoso
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMTazameni Miujiza (Vol 2)
CATEGORYZaburi
REFMt. 5
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
4
SOURCETanzania
 • Comments