Heri Walio Maskini
Heri Walio Maskini Lyrics
- {Heri walio maskini wa roho,
Kwa maana ufalme wa mbinguni ni wao }*2
{(Heri) heri wenye huzuni (wao) watafarijiwa
(Heri) wenye upole watairithi nchi }*2
- Heri walio na njaa na kiu ya haki,
Kwa maana maana hao watashibishwa (heri)
Heri wenye rehema (hawa) watapata rehema
Heri wenye moyo safi hao watamwona Mungu
- Heri wale walio wapatanishi
Kwa maana wataitwa wana wa Mungu
(Heri) wenye kuuliwa (kwa) kwa ajili ya haki
kwa maana ufalme wa mbinguni ni wao
- Heri washutumiwao na kuudhiwa,
Na kunenewa neno baya kwa ajili yangu *2
(Nyinyi) furahini sana (pia) na kushangilia
Kwa maana dhawabu yenu ni kubwa mbinguni