Hii Ndiyo Siku
| Hii Ndiyo Siku | |
|---|---|
| Performed by | Our Lady of Fatima Kongowea |
| Album | Kila Mwenye Pumzi (vol 4) |
| Category | Entrance / Mwanzo |
| Views | 10,184 |
Hii Ndiyo Siku Lyrics
Hii ndiyo siku, aloifanya Bwana *2
Tuishangilie, na kuifurahiya *2
{Tupige makofi na vigelegele
Sote turuke juu tumshukuru Mungu } *2- Ndiwe Mungu wangu nami nitakushukuru
Ndiwe Mungu wangu nami nitakutukuza
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
Kwa mema yote Bwana uliyonijalia - Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia mimi na kumshukuru Mungu
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
Kwa mema yote Bwana uliyonijalia - Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa
Mkono wa Bwana hutenda makuu
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
Kwa mema yote Bwana uliyonijalia - Mshukuruni Bwana kwa kuwa yeye ni mwema
Kwa maana fadhili zake ni za milele
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote
Kwa mema yote Bwana uliyonijalia