Hii ni Ekaristi
   
    
     
         
          
            Hii ni Ekaristi Lyrics
 
             
            
- Hii ni ekaristi, aliyotuachia
 Bwana Yesu Kristu (Kristu)
 Mkombozi wa dunia
 { (imbeni) Imbeni kwa furaha
 (sifuni) Sifuni ekaristi
 (alimo) Alimo Yesu Kristu (Kristu)
 Alimo ni mzima } *2
- Yesu katuonea, wema pia huruma
 Alitupenda sana (sana)
 Akatupa uzima
- Jioni Alhamisi, alichukua mkate
 Kaugeza mwili (mwili)
 Kuleni mkaokoke
- Pia alichukua, kikombe cha divai
 Kaigeuza damu (damu)
 Kunyweni mkaokoke
- Walipokwisha kula, kawaosha miguu
 Nimewapa mfano (mfano)
 Fanyeni nanyi vile
- Yesu mwili na damu, chakula cha uzima
 Tujaliwe kupata (pata)
 Uzima wa milele.