Hii ni Karamu
Hii ni Karamu Lyrics
Hii ni karamu, uzima wa roho,
Yumo Bwana Yesu, kwa mwili wake, kweli na damu yake
- Alisema Bwana twaeni wote, mle ni mwili wangu
- Alisema Bwana twaeni wote, mnywe ni damu yangu
- Nasi twasadiki ni mwili wake, kweli na damu yake
- Alituamuru kufanya hivyo, kwa ukumbusho wake
- Tukifanya hivyo tunatangaza, kifo cha Bwana Yesu
- Kwa hii karamu, Twashiriki uzima wa Bwana wetu
- Huu ni upendo aliotuachia, mkombozi wetu
- Hapa duniani twaishi na Baba, kwa karamu hii
- Na huko mbinguni tutaishi, na Baba milele yote