Hiki Ndicho Chakula Bora Lyrics

HIKI NDICHO CHAKULA BORA

@ Deo Kalolela

{ Hiki ndicho chakula bora kwa wanyofu wa moyo
Wote wenye mioyo safi Bwana awaalika } *2
{ /s/ a/t/b/
Haya njoni wote mezani kwa chakula bora cha uzima
Haya njoni wote mezani kwa chakula bora
Haya njoni kwa chakula bora, cha uzima
Wana heri wale wote, wanaokipokea } *2

  1. Kwa upendo Bwana Yesu amejitoa kama chakula
    Bwana akajitoa, apate kuziokoa roho zetu.
  2. Njooni wote wenye kiu ya kupokea wokovu wake
    Njooni maskini, njoni viwete vipofu na wagonjwa
  3. Tule tunywe siku zote kwa ukombozi wa roho zetu
    Haya njoni wote, mezani kwa Bwana kwa chakula bora
Hiki Ndicho Chakula Bora
COMPOSERDeo Kalolela
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMilele Milele Msifuni (Vol 1)
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
MUSIC KEYA Flat Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF
  • Comments