Hodi Hodi Nyumbani

Hodi Hodi Nyumbani
Performed bySt. Joseph Migori
AlbumHodi Hodi
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerAlfred Ossonga
Views32,053

Hodi Hodi Nyumbani Lyrics

  1. Hodi hodi nyumbani mwako Bwana, ninabisha nifungulie
    Nimekuja nyumbani mwako leo, nimekuja kukuabudu,
    Kwa unyenyekevu naijongea, meza yako yenye baraka
    Nakuja na sala zangu Ee Bwana, nakuomba zisikilize
    Ninakutolea sadaka safi, Mungu Baba uipokee.

  2. [ b ] Nyua za Bwana zapendeza, zinapendeza macho kama nini
    Natamani kuingia hekaluni, [ w ] nikamwabudu
  3. Nimeingia hekaluni, nimeingia hekaluni mwako
    Nimekuja kuabudu kusujudu, nyumbani mwako
  4. Unipokee Mungu wangu unitakase, mimi mwenye dhambi
    Nimekuja mbele zako Mungu Baba, unipokee