Hubirini Viumbe Vyote
Hubirini Viumbe Vyote Lyrics
- Hubirini viumbe vyote muishio duniani
Tangazeni wokovu wake muumba mbingu na nchi
Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba
Kwa mfano na sura yake Mungu wetu
Hubirini kwa kuimba tena kwa kusali na kucheza
Tangazeni utukufu wake aliye mtawala, Semeni
kwa shangwe pia na furaha Bwana ni mtawala
Ametukomboa ametubariki njooni tufurahi naye
- Tukuzeni sifa zake enyi viumbe wa duniani
Wahubiriini mataifa habari za utukufu
Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba
Kwa mfano na sura yake Mungu wetu
- Na nyimbo nzuri na pia shangwe asifiwe Mwokozi
Shamra shamra vigelegele asifiwe Mwokozi
Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba
Kwa mfano na sura yake Mungu wetu
- Vilema bubu na viziwi wote wapone leo
Matajiri na maskini wote waungane pamoja
Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba
Kwa mfano na sura yake Mungu wetu
- Watu wote na wasimame washikane mikono
Watoto nao kwa pamoja tuwainue juu
Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba
Kwa mfano na sura yake Mungu wetu