Huruma Bwana
| Huruma Bwana | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | (traditional) |
| Views | 8,293 |
Huruma Bwana Lyrics
Huruma Bwana, huruma kwa watu wako
Uliowakomboa kwa damu yako takatifu *2- Ee Mungu unirehemu,
Sawa sawa na fadhili zako. - Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu. - Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu. - Ee Mungu uniumbie moyo safi,
Uifanye upya roho uliyotulia ndani yangu. - Usinitenge na uso wako,
Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee.