Huyu Ni Yule Yesu
Huyu Ni Yule Yesu | |
---|---|
Performed by | St. Joseph Migori |
Album | Uzuri wa Yesu |
Category | Jumapili ya Matawi (Palm Sunday) |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 16,591 |
Huyu Ni Yule Yesu Lyrics
Huyu ni yule Yesu, Yesu mwana wa Daudi
Huyu ni yule Yesu, Mwana wa Galilaya- Mwambieni Binti Sayuni, tazama mfalme wako
Anakuja kwako mpole amepanda mwanapunda*2 - Inukeni enyi malango, inueni vichwa vyenu
Mfalme apate ingia, mfalme wa utukufu *2 - Na watoto wa Wayahudi, Walimlaki Mwokozi
Wakiyachukua matawi, wakipiga makelele *2 - Aliyakemea mawimbi, Bahari ikatulia
Akatembea juu ya maji, akatembea kwa miguu*2 - Aliponya wagonjwa wengi kwa neno la kinywa chake
Hata vazi lake ni dawa, yule mama alipona *2 - Alimfufua Lazaro, Lazaro aliyekufa
Akarudi tena mzima akatoka kaburi *2
Recorded by
* St. Joseph Migori (Uzuri wa Yesu album)
* St. Kizito Makuburi Dsm (Nyumba ya Roho album)