Huyu Ni Yule Yesu

Huyu Ni Yule Yesu
ChoirSt. Joseph Migori
AlbumUzuri wa Yesu
CategoryJumapili ya Matawi (Palm Sunday)
ComposerAlfred Ossonga
Musical Notes
Timesignature2 4
MusickeyD Major
NotesOpen PDF

Huyu Ni Yule Yesu Lyrics

Huyu ni yule Yesu, Yesu mwana wa Daudi
Huyu ni yule Yesu, Mwana wa Galilaya1. Mwambieni Binti Sayuni, tazama mfalme wako
Anakuja kwako mpole amepanda mwanapunda*2

2. Inukeni enyi malango, inueni vichwa vyenu
Mfalme apate ingia, mfalme wa utukufu *2

3. Na watoto wa Wayahudi, Walimlaki Mwokozi
Wakiyachukua matawi, wakipiga makelele *2

4. Aliyakemea mawimbi, Bahari ikatulia
Akatembea juu ya maji, akatembea kwa miguu*2

5. Aliponya wagonjwa wengi kwa neno la kinywa chake
Hata vazi lake ni dawa, yule mama alipona *2

6. Alimfufua Lazaro, Lazaro aliyekufa
Akarudi tena mzima akatoka kaburi *2
Recorded by * St. Joseph Migori (Uzuri wa Yesu album) * St. Kizito Makuburi Dsm (Nyumba ya Roho album)

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442