Huyu ni Yule Yesu
Huyu ni Yule Yesu | |
---|---|
Performed by | St. Kizito Makuburi |
Album | Nyumba ya Roho |
Category | Jumapili ya Matawi (Palm Sunday) |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 6,690 |
Huyu ni Yule Yesu Lyrics
Huyu ni yule Yesu, [t] Yesu
Yesu mwana wa Daudi
Huyu ni yule Yesu, [s] Yesu
Mwana wa Galilaya- Mwambieni Binti Sayuni, tazama mfalme wako
(Anakuja kwako mpole, amepanda mwanapunda*2) - Inukeni enyi malango, inueni vichwa vyenu
(Mfalme apate ingia, mfalme wa utukufu *2) - Na watoto wa Wayahudi, walimlaki Mwokozi
(Wakiyachukua matawi, wakipiga makelele *2) - Aliyakemea mawimbi, bahari ikatulia
(Akatembea juu ya maji, akatembea kwa miguu *2) - Aliponya wagonjwa wengi, kwa neno la kinywa chake
(Hata vazi lake ni dawa, yule mama alipona *2) - Alimfufua Lazaro, Lazaro aliyekufa
(Akarudi tena mzima akatoka kaburini *2)