Ikulu ya Mbinguni
   
    
     
         
          
            Ikulu ya Mbinguni Lyrics
 
             
            
- { Ukimcha Bwana Mungu (katika) maisha yako yote
 Hakika utakaribishwa (kwenye) ikulu ya Mbinguni } *2
- Tazama Mungu ni hodari (sana) wala hamdharau mtu yeyote
 Naye ana uwezo (mwingi) katika kufunza ufahamu mwingi
- Hufungua masikio (yako) yasikie maonyo yake mwenyezi
 Na kukuagiza (urudi) kwake na kuuacha uovu wako wote
- Kama wewe ukisikia (wewe) na kumtumikia atapitisha siku zako
 Na mafanikio (mengi) na miaka yenu katika furaha
- Na ukithamini zaidi (mali) kuliko roho yako utaangamia
 Na kufaa pasipo (maarifa) hautauona uso wa Mungu
- Basi jitunze isije (hasira) ikakuvuta ama ukafanya mzaha
 Wala usikubali (kamwe) ukuu wa ukombozi ukutawale