Ikulu ya Mbinguni

Ikulu ya Mbinguni
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumIkulu ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerM. Z. Yohana

Ikulu ya Mbinguni Lyrics

{ Ukimcha Bwana Mungu (katika) maisha yako yote
Hakika utakaribishwa (kwenye) ikulu ya Mbinguni } *2

 1. Tazama Mungu ni hodari (sana) wala hamdharau mtu yeyote
  Naye ana uwezo (mwingi) katika kufunza ufahamu mwingi
 2. Hufungua masikio (yako) yasikie maonyo yake mwenyezi
  Na kukuagiza (urudi) kwake na kuuacha uovu wako wote
 3. Kama wewe ukisikia (wewe) na kumtumikia atapitisha siku zako
  Na mafanikio (mengi) na miaka yenu katika furaha
 4. Na ukithamini zaidi (mali) kuliko roho yako utaangamia
  Na kufaa pasipo (maarifa) hautauona uso wa Mungu
 5. Basi jitunze isije (hasira) ikakuvuta ama ukafanya mzaha
  Wala usikubali (kamwe) ukuu wa ukombozi ukutawale