Uje Roho Mtakatifu Tuangaze
Uje Roho Mtakatifu Tuangaze | |
---|---|
Performed by | St. Augustine Bugando Mwanza |
Category | Roho Mtakatifu (Pentecoste) |
Composer | (traditional) |
Views | 109,225 |
Uje Roho Mtakatifu Tuangaze Lyrics
- Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu
Roho zetu kwa mwangao - Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji
Uje mwanga wa mioyo - Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana
Ewe raha mustarehe - Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto, burudiko
U mfutaji wa machozi - Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini
Neema yako mioyoni - Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu
Kwake yote yana kosa - Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu
Na kuponya majeraha - Ulegeze ukaidi, washa moto wa uadili
Nyoosha upotevu wote - Wape waumini wako, wenye tumaini kwako
Paji zako zote saba - Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila
Wape heri ya milele - Amina aleluya, amina aleluya,
Amina aleluya