Uje Roho Mtakatifu Tuangaze Lyrics

UJE ROHO MTAKATIFU TUANGAZE

@ (traditional)

 1. Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu
  Roho zetu kwa mwangao
 2. Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji
  Uje mwanga wa mioyo
 3. Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana
  Ewe raha mustarehe
 4. Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto, burudiko
  U mfutaji wa machozi
 5. Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini
  Neema yako mioyoni
 6. Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu
  Kwake yote yana kosa
 7. Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu
  Na kuponya majeraha
 8. Ulegeze ukaidi, washa moto wa uadili
  Nyoosha upotevu wote
 9. Wape waumini wako, wenye tumaini kwako
  Paji zako zote saba
 10. Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila
  Wape heri ya milele
 11. Amina aleluya, amina aleluya,
  Amina aleluya
Uje Roho Mtakatifu Tuangaze
COMPOSER(traditional)
CHOIRSt. Augustine Bugando Mwanza
CATEGORYRoho Mtakatifu (Pentecoste)
MUSIC KEYF Major
TIME SIGNATURE6
8
SOURCETanzania
 • Comments