Isemavyo Torati
Isemavyo Torati | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Mshike Mshike (Vol 5) |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 3,846 |
Isemavyo Torati Lyrics
{ Isemavyo torati ya kale, jicho kwa jicho, jino kwa jino
Mkuki kwa mkuki, hiyo silaha ya mababu } *2
{ Lakini mimi, ninawaambia, nawaambia,
Msilipize kisasi kwa mambo haya } *2
Akupigaye shavu lako moja, mgeuzie na la pili
Akunyang'anyaye na joho lako -
Mpe pia kanzu yako, utayashinda majaribu.- Ndugu nawaambia nyinyi, jifunzeni kusameheana
Acheni chuki ubinafsi, hazisaidii kwa vyovyote.
Ukikosewa samehe, sababu hata wewe wakosea
Mungu asingesamehe, wewe na mimi tungekuwa wapi - Wewe unayemchukia huyu, huyu ameumbwa naye Mungu
Kumbuka wote sisi twapita, hakuna aishiye milele
Wamuua huyu na wewe, utakufa siku moja kama yeye
Utajibu nini kwa Mungu, kuifanya kazi yake bila ruhusa - Riziki aitoa Mungu, acha wivu pia masengenyo
Mwenzako amepata kwa jasho, fanya bidii ufanikiwe
Wamwonea wivu kwa nini, na kuanza kuharibu na kuiba
Utajibu nini kwa Mungu, kuharibu nchi yake aliyoumba