Isemavyo Torati

Isemavyo Torati
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMshike Mshike (Vol 5)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,698

Isemavyo Torati Lyrics

  1. { Isemavyo torati ya kale, jicho kwa jicho, jino kwa jino
    Mkuki kwa mkuki, hiyo silaha ya mababu } *2
    { Lakini mimi, ninawaambia, nawaambia,
    Msilipize kisasi kwa mambo haya } *2

    Akupigaye shavu lako moja, mgeuzie na la pili
    Akunyang'anyaye na joho lako -
    Mpe pia kanzu yako, utayashinda majaribu.

  2. Ndugu nawaambia nyinyi, jifunzeni kusameheana
    Acheni chuki ubinafsi, hazisaidii kwa vyovyote.
    Ukikosewa samehe, sababu hata wewe wakosea
    Mungu asingesamehe, wewe na mimi tungekuwa wapi
  3. Wewe unayemchukia huyu, huyu ameumbwa naye Mungu
    Kumbuka wote sisi twapita, hakuna aishiye milele
    Wamuua huyu na wewe, utakufa siku moja kama yeye
    Utajibu nini kwa Mungu, kuifanya kazi yake bila ruhusa
  4. Riziki aitoa Mungu, acha wivu pia masengenyo
    Mwenzako amepata kwa jasho, fanya bidii ufanikiwe
    Wamwonea wivu kwa nini, na kuanza kuharibu na kuiba
    Utajibu nini kwa Mungu, kuharibu nchi yake aliyoumba