Harusi Yetu Leo
| Harusi Yetu Leo | |
|---|---|
| Alt Title | Jamani Leo ni Furaha | 
| Performed by | Our Lady of Fatima Kongowea | 
| Album | Kila Mwenye Pumzi (vol 4) | 
| Category | Harusi | 
| Views | 8,855 | 
Harusi Yetu Leo Lyrics
- { Jamani leo ni furaha,
 Leo leo kwetu sisi ni furaha, furaha } *2Harusi yetu leo tuishangilie,
 hongera kwenu, tunawapa heko
 Wapenzi wametuita tuwape heko,
 hongera kwenu, tunawapa heko,
 { Nazo baraka zake Mungu ziwe nanyi pia,
 maishani mwenu } *2
- Mimi nimekuchagua uwe wangu wa maisha,
 Naahidi takupenda siku zote milele.
- Mimi kweli nitakupenda kwa roho yangu yote,
 Kama vile Yesu alivyoipenda kanisa
- Angalia vazi langu lilivyopambwa marembo,
 Hata ndege wa angani wanatushangilia.
- Mwendo wako wa maringo, sura yako ya mapenzi,
 Mungu Baba atujalie baraka milele
 
  
         
                            