Jicho Langu

Jicho Langu
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumMchanganyo
CategoryTafakari
ComposerFelician Bukene
Views6,519

Jicho Langu Lyrics

  1. Ni wewe jicho langu nakutegemea kuniongoza (niendapo)
    Ni wewe jicho langu taa yangu ya kumulika njia (nipitayo)
    {Niongoze kwa huruma, niongoze kwa mapendo
    Nitazame mambo mema, yanayopendeza Mungu
    Jicho langu niongoze hata nikafike kwa Mungu Baba}

  2. Ukiwaona vipofu wote – tazama kwa huruma
    Na ukiwaona walemavu wote . . .
    Na ukiwaona wasiojiweza . . .
    Nikafike kwake Mungu kwa huruma yangu
  3. Ukiwaona yatima wote – tazama kwa huruma
    Na ukiwaona na wajane pia . . .
    Na ukiwaona wanaoonewa . . .
    Nikafike kwake Mungu kwa huruma yangu
  4. Mwenendo mbaya wa binadamu – hayo usitazame
    Kama tamaa anasa ushirikina . . .
    Na matendo yanayomuasi Mungu . . .
    Nikafike kwake Mungu kwa matendo mema
  5. Pia unapowaona wahitaji – tazama kwa upendo
    Na kila mwanadamu aliyeumbwa . . .
    Haja za familia uliyonayo . . .
    Nikafike kwake Mungu kwa upendo wangu