Jinsi Lilivyo Tukufu Lyrics

JINSI LILIVYO TUKUFU

@ J. C. Shomaly

NIKIZIANGALIA MBINGU

{ Wewe Bwana Mungu wetu
Jinsi lilivyo tukufu (jina)
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote } * 2
Nikiziangalia mbingu ni kazi yako Bwana
Mwezi pia na nyota ulizoratibisha wewe
Naona ajabu ajabu ajabu *2

  1. Naye mtu ni nini Bwana, hata umkumbuke
    Na binadamu hata yeye umwangazie
  2. Kondoo nao ng'ombe pia wanyama wa kondeni
    Ndege pia samaki ndani ya bahari
  3. Umemfanya punde punde mdogo kuliko Mungu
    Umemvika taji taji ya heshima
Jinsi Lilivyo Tukufu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRHoly Trinity Kariobangi
ALBUMMaisha Yangu
CATEGORYZaburi
REFPs. 8
  • Comments