Jipe Moyo
| Jipe Moyo | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 16,053 | 
Jipe Moyo Lyrics
- Jipe moyo Bwana yuko nawe, (tena)
 Hakuachi kamwe kwani yeye akupenda
 Hata shida zikikuandama (ndugu)
 Umtegemee, Yesu atakuongoza
- Njia imejaa giza na umande,
 Huku watembea bila hata nuru wasi wasi
 Hofu yakujaa woga watawala
 Wasimama wima hujui pa kwenda
 Ushujaa watoka wabaki upweke,
 Bali yu pamoja na wewe
- Ndugu watoweka wakuacha pweke,
 Hata marafiki uliothamini watoroka
 Hofu yakujaa woga watawala
 Wasimama wima hujui pa kwenda
 Ushujaa watoka wabaki upweke,
 Bali yu pamoja na wewe
- Kila utendacho, hakiwezekani,
 Wajaribu sana kufaulu wala hauwezi
 Hofu yakujaa woga watawala
 Wasimama wima hujui pa kwenda
 Ushujaa watoka wabaki upweke,
 Bali yu pamoja na wewe
 
  
         
                            