Jipe Moyo

Jipe Moyo
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Jipe Moyo Lyrics

Jipe moyo Bwana yuko nawe, (tena)
Hakuachi kamwe kwani yeye akupenda
Hata shida zikikuandama (ndugu)
Umtegemee, Yesu atakuongoza

 1. Njia imejaa giza na umande,
  Huku watembea bila hata nuru wasi wasi
  Hofu yakujaa woga watawala
  Wasimama wima hujui pa kwenda
  Ushujaa watoka wabaki upweke,
  Bali yu pamoja na wewe
 2. Ndugu watoweka wakuacha pweke,
  Hata marafiki uliothamini watoroka
  Hofu yakujaa woga watawala
  Wasimama wima hujui pa kwenda
  Ushujaa watoka wabaki upweke,
  Bali yu pamoja na wewe
 3. Kila utendacho, hakiwezekani,
  Wajaribu sana kufaulu wala hauwezi
  Hofu yakujaa woga watawala
  Wasimama wima hujui pa kwenda
  Ushujaa watoka wabaki upweke,
  Bali yu pamoja na wewe