Kama Kunguru
Kama Kunguru | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Habari Tuliyoleta (Vol 6) |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 4,643 |
Kama Kunguru Lyrics
{ Kama kunguru arukapo juu ya jalala kubwa
Akitafuta mizoga na wadudu
Alishibishe tumbo lake } *2
{ Ndivyo moyo wake mtu asiyempenda Mungu
Utakuwa wa kubabaika na kuhangaika
Hatakuwa na amani,
Atakuwa kama kunguru tu, kama kunguru tu,
Awindaye toka macheo ya jua hata yapata mawio
Na tumbo lake bado ni tupu } *2- Moyo wako ndugu mbona waubabaisha,
Kutwa kucha wewe umemsahau Mungu
Dunia ina mambo yake - tena yanapita - Kama una kiu na tamaa za dunia
Zina mwisho wake kwanza mtafute Mungu
Mungu alishapanga yako - hivyo umuombe