Karibuni Watu Wote
Karibuni Watu Wote Lyrics
[s] Karibuni watu wote--
[w]Twende kwake Bwana Yesu
[s] Tujongee mbele zake--
[w] Tumwabudu Mungu wetu
[t] Aai aiya--
[s] Twende wote kwa furaha tupige vigelegele
[w]Tumwimbie Mungu wetu
- Kama si uwezo wake hatungepata uhai
Alleluia--atukuzwe Mungu wetu
Kama si uwezo wake hatungekuwa na nguvu
- Wana wako Bwana Mungu tumekuja mbele zako
Alleluia--atukuzwe Mungu wetu
Twakuomba ewe Mungu upokee sala zetu
- Kina mama kina baba tumsifu Mungu wetu
Alleluia--atukuzwe Mungu wetu
Na wazee kwa vijana tumsifu Mungu wetu