Kazi ya Vidole
Kazi ya Vidole Lyrics
NIKIZIANGALIA MBINGU
Nikiziangalia Mbingu, kazi ya vidole vyako
Mwezi nyota ulizoziratibisha,
(Mtu ni kitu gani (mtu ni) hata umkumbuke
Na binadamu hata umwangalie *2)
- Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu
Umemfika taji ya utukufu na heshima
Umemtawaza juu ya kazi ya mikono yako
Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
- Kondoo na ng'ombe wote, na ng'ombe wote pia
Naam na wanyama wa kondeni, wa kondeni
Ndege wa angani na samaki wa baharini,
Na kila kipitacho njia za baharini.
- Wewe Mungu Bwana wetu Mungu Bwana wetu
Jinsi lilivyotukufu jina lako duniani
Wewe umeweka utukufu wako Mbinguni
Vinywani mwa watoto umeweka misingi
- Kwa sababu yao wanaoshindana na wewe,
Uwakomeshe adui na kulipa kisasi
Mtu kitu gani hata wewe umkumbuke
Na binadamu hata umwangalie