Kidole Juu
Kidole Juu | |
---|---|
Alt Title | Nitumwe Mimi |
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Kidole Juu (Vol 23) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 26,746 |
Kidole Juu Lyrics
- //utangulizi//
Hayo mliyofunuliwa, bila kuyalipia kitu,
Nayo ndiyo yale mliyotumwa,
Kwenda kwa walio wadogo
Mungu alowatunukia awe mkuu peke yake
(Jiulize) nani kwenu (aliyeomba) kuzaliwa!
(Jiulize tena) nani kwenu (anayejua) siku ya kufa!
Hakuna! Hakuna! ha!Hakuna jambo mnalomiliki hapa duniani
Yote mliyo nayo yana mwenyewe mnamjua
Naye amewapa haya kusudi mtumikiane
Ili kusiwepo na matabaka miongoni mwenu
Hiyo ndiyo hekima - eeh aah eeh
Hiyo ndiyo hekima - eeh aah eeh
Ndugu hiyo ndiyo hekima ya kweli } *2 - Kama mliyo nayo yote yangekuwa yenu
Hiyo pumzi mnayojivunia wapendwa,
Isingekuwa inakiogopa kichomi
Ingeendele-a hata palipo kichomi! - Uzuri wa sura zenu zenye ngozi laini
Inakuwaje hamuwezi kuuelekeza,
Usiungue hata kwenye maji ya moto
Na usioze unapolala kaburini! - Elimu na vyeo vyenu na mamlaka yenu
Akili nyingi ufundi navyo vipaji vyenu,
Mbona hamvitumii nyi mkiwa usingizini
Na mnaota ndoto sawa na za watoto!
//hitimisho//
Basi mimi, ninahimizwa, kujiepusha, kujiinua
Nijishushe, mbele ya wote,
Wawe wakubwa, au wadogo
Nisijiinue kati ya watu hata siku moja,
Badala yake nijinyenyekeze ili nifikike,
Akihitajika atakayewatumikia watu
Niinue kidole juu kusudi wanitume mimi, daima
Kidole juu kusudi wanitume mimi
Kidole juu, kuitikia wito daima
Kidole juu, kusudi wanitume mimi
Na nikitumwa niwe mwaminifu daima
Kidole juu, kusudi wanitume mimi
Kidole juu wanitume na Mungu atukuzwe daima
Kidole juu, kusudi wanitume mimi
Kidole juu, kidole juu, leo
Kidole juu, kusudi wanitume mimi
Kidole juu, kidole juu, daima
Kidole juu, kusudi wanitumie mimi, milele!
Second version of this song is Nitumwe Mimi, that replaces the words 'Kidole Juu kusudi wanitume mimi' with 'nijitokeze kusudi wanitume mimi'
And alters the title to 'Nitumwe Mimi'