Kila Kunapokucha
Kila Kunapokucha |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 4,117 |
Kila Kunapokucha Lyrics
{ Kila kunapokucha, ndugu zangu mimi
Wananikwepa na kunikimbia
Majirani zangu wanatazamana bila kunitamkia neno
Ewe Muumba wangu najiuliza na kujitafakari mimi
Au nimekuwa na sura ya simba,
Au nimekuwa na sura ya chui, hata ninatisha } *2
- Ninapokaa chini na kutafakari mwenendo wangu
Kwani uko vipi mimi niliupenda,
Japo magumu mimi niliyapata,
Nilivaa sura ya kifalme pasipo kuwa na utu
- Nikiupekua pekua moyo wangu unanitisha
Ni huo tena kwa kudhamiria
Kwa kauli toka kwa ulimi wangu
Nilifanana na jitu baya tena limezalo watu
- Hakuna adui hakuna rafiki kwangu wote sawa
Hakuna mwema katika moyo wangu
Wala rafiki katika roho yangu
Nilijifananisha na chui tena chui mwenye njaa