Kimya ni Cha Nini
Kimya ni Cha Nini Lyrics
Kimya kimya ni cha nini Bwana Yesu ametualika
Kushiriki karamu yake, karamu ya mapendo
Siku ile iliyotangulia kifo chake
(Aliwaita wanafunzi wake) *2 akawaambia
- Huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu
Kuleni huu ili mpate uzima wa milele,
(Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeni
kushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2
- Hii ndiyo damu yangu itakayotolewa kwa ajili yenu
Kunyweni hii ili mpate uzima wa milele
(Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeni
kushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2
- Amini ninawaambieni alaye mwili na kunywa damu
Bila kustahili atahukumiwa siku ya mwisho,
Lakini alaye mwili na kunywa damu kwa kustahili
Nitamfufua siku ya mwisho
(Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeni
kushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2