Kina Hiki

Kina Hiki
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerJ. C. Shomaly
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyG Major

Kina Hiki Lyrics

Kina hiki kina maji mengi pande nne zimejaa, ee Bwana,
Dunia nayo mji mkavu, wamemezwa watu wengi ee Bwana
(Ona) watu wauana ovyo,(ona) vita navyo vimezidi
(Tena) magonjwa ya kushangaza
Sasa Bwana tufanyeje sisi?

{ Tunalia tunalia Bwana twalilia ulimwengu huu
Na machozi yetu sisi Bwana yakiokoe kizazi hiki
Usimame tutetee Bwana tusaidie wanao } *2

  1. Maji yamekuwa mengi sana nashindwa kuvumilia,
    Sina msaada mimi Bwana naomba nihurumie
  2. Shida nyingi sana mimi Bwana zinazidi kunisonga,
    Nashindwa kuvumilia mimi ee Mungu nihurumie
  3. Dunia nayo yahuzunisha maovu yametawala,
    Watu nao wateseka sana ee Mungu tusaidie