Kisha Nikaona
| Kisha Nikaona | |
|---|---|
| Performed by | St. Joseph Migori | 
| Album | Mabawa | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Composer | Alfred Ossonga | 
| Views | 14,316 | 
Kisha Nikaona Lyrics
- Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya
 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya
 { Nikauona mji (mji ule), ule mtakatifu
 Jerusalem mpya ukishuka toka mbinguni } *2
- Kwa maana mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza,
 Zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena
- Nikasikia sauti kubwa ikitoka,
 Kwenye kiti cha enzi, tazama maskani yake Mungu
- Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao,
 Naye atayafuta, machozi katika macho yao
- Mauti maombolezo kilio maumivu,
 Hayatakuwapo, tazama yote yamekuwa mapya
 
  
         
                            