Kisha Nikaona

Kisha Nikaona
ChoirSt. Joseph Migori
AlbumMabawa
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerAlfred Ossonga

Kisha Nikaona Lyrics

Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya
{ Nikauona mji (mji ule), ule mtakatifu
Jerusalem mpya ukishuka toka mbinguni } *2

 1. Kwa maana mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza,
  Zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena
 2. Nikasikia sauti kubwa ikitoka,
  Kwenye kiti cha enzi, tazama maskani yake Mungu
 3. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao,
  Naye atayafuta, machozi katika macho yao
 4. Mauti maombolezo kilio maumivu,
  Hayatakuwapo, tazama yote yamekuwa mapya