Kristu Yeye Yule

Kristu Yeye Yule
Choir-
CategoryKristu Mfalme (Christ the King)
ComposerJ. C. Shomaly
SourceKaani Machakos

Kristu Yeye Yule Lyrics

{ Kristu yeye yule leo na milele,
Huyu Yesu Yeye ndiye Alfa na Omega, Kristu }*2
{ Ni mwanzo wa (nyakati), ni mwisho wa (nyakati)
Jana leo (na kesho), Alfa pia (Omega)
Tawala tawala tawala Kristu, tawala mioyo yetu } *2

 1. Wewe ndiwe kitulizo cha maisha yetu, Kristu
  Wewe ndiwe mkate wetu wa kila siku, Kristu
 2. Ukombozi umetupa kwa kunyenyekea, Kristu
  Tutakupa nini kama fidia ya kweli Kristu, Kristu
 3. Ugumu wa ulimwengu wanipa vikwazo, Kristu
  Natamani kufanana na rafiki zangu, Kristu
 4. Nijalie maisha mema yenye baraka, Kristu
  Nipate ninayopenda kwa mapenzi yako, Kristu
 5. Nijalie moyo wa kutopenda tamaa, Kristu
  Nitosheke na yote utayonipa mimi, Kristu